Tel: +255752115528| Mail: info@elctmwd.org




USHARIKA WA KISANGARA

Mtaa wa Kisangara ulianzishwa mwaka 1947 kabla ya kuwa mtaa mwaka 1925 alibatizwa mkristo wa kwanza anayeitwa Mbatia Chidua alipobatizwa akaitwa Petro Chidua. Mwaka 1928 walibatizwa wakristo 12 ikiwa ni awamu ya sita ya waliobatizwa wakati huo katika eneo la Kiruru. Eneo la Kisangara kulikuwepo wakristo watatu wakaungana pamoja na wakristo wa Kiruru wakasali usharika wa Shighatini chini ya Mchungaji Simioni Mbatiani na walipoongezeka kidogo wakaanza kusali Kiruru wakiongozwa na Mwinjilisti Marthin Kaduri
Mtaa wa kisangara ulizaliwa toka usharika wa Usangi 1947

Mtaa huu ulikuwa unaongozwa na mwinjilisti Naftali Aserry , Mchungaji akiwa ni Nathanael Mgaya aliyekuwa ni mchungaji wa Usangi , baada ya mwinjilisti Naftali Aserry kurudi Usangi ibada za jumapili zikaendeshwa na wainjilisti toka Usangi kwa zamu ambao ni Sefania Charokiwa na Yohane Marisa na siku zenye sakramenti na ubatizo Mchungaji Nathanaeli Mgaya , Eliewaha Mshana na Erinesti Mhando walikuwa wakishuka kutoka Usangi kuhudumia.
Mwaka 1974 alichaguliwa mwinjilisti Martini Kaduri kuongoza mtaa wa kisangara.
Ndio “bush bchool” ilikuwepo na walimu waliokuwa wakifundisha ni Naftali Asery kutoka Usangi, Mr Shughuru pamoja na Mr. Msechu kutoka kifula.Jengo hilo lilitumika pia kwa kufanyia ibada. Usharika wa usangi ulisaidia ujenzi wa “bush school” kiasi cha shilingi 171 pamoja na Milango, Madirisha na Madawati kwa miaka hiyo ya nyuma.

Waanzilishi wa mtaa wa Kisangara kabla ya kuwa usharika kamili ni pamoja na;-
Petro Chidua
Simon Kiraghinja
Marthin Kaduri
Abrahamu Kakola
Mama Lonaya
Asinati Kimomwe
Shedrack Kangero
Stefano Shedrack Kangero
William Charles Msengo
Natujael Hendrish Sangiwa.

Watu wa kwanza kubatizwa katika mtaa huo ambao kwa sasa ni Usharika kamili ni;- Petro Chidua ,Mama Lonaya, Marthin Kaduri,Elina Salimu,Stefano Shedraki, Wiliamu Charles, Natujaeli Hendrish.
Baada ya mtaa wa Kisangara kuwa Usharika hawa ndio watumishi walio ongoza pamoja nakutoa huduma.
Wainjilisti:-
Betueli Kitundu.
Msafiri Tulo.
Elimiliki Mbaga.
Elangwa Mbwambo.
Lameck Mmbaga.
Elifather .
Davidi Msuya.
Santoni Msuya.
Aron Lema.
Witiness Apendaeli Mchome.

Wachungaji walio toa huduma wakati Kisangara ikiwa chini ya Usharika wa Kilevo/Kileo ni:-
Mch. Isaya Melita.
Mch. Yameti Mbulu.
Mch. Aminieli Kisaka.
Mch. Seth Mzava.
Mch. Moses Tezura.
Mch. Sauli Ndoveni.

Usharika wa Kisangara ulizaliwa kutoka mtaa kipindi cha Mch. Sauli Ndoveni mwaka 1980 na Mchungaji wa kwanza wa Kisangara akawa Mch. Samweli Mzirai.
Hawa ndio wachungaji wa usharika wa Kisangara ulipozaliwa
Mch. Samweli Mzirai 1980 - 1985
Mch. Habart Sila Msangi 1986 - 1992
Mch. Sauli Ndoveni 1993 – 1995
Mch. Danieli Mzava 1995 - 2000
Mch.Sauli Ndoveni 2000 - 2001
Mch.Frank Kilango 2001
Mch. Spiker Urio 2002
Mch. Davidi P Aseri 2003 - 2006
Mch. Godson Mshana 2006 - 2008
Mch. Elinkanleka Mlemba 2008 -2009
Mch. Joyce R Muze 2010 -2018
Mch .Charles E Tenga 2019 ~


MCHUNGAJI

MCHG. MBONEA MFWANGAVO


USHARIKA WA KISANGARA



JIMBO USHARIKA PASTOR (MCHUNGAJI)       CONTACT           STREETS (MITAA)
JIMBO LA TAMBARARE KISANGARA MCHG. MBONEA MFWANGAVO 0758 419 471 Kisangara, Kiruru na Lembeni

  GO HOME        GO BACK