
WOTE WAWE NA UMOJA: YOHANA 17:21 / 6 NOVEMBA 2016
Katika Dayosisi ya Mwanga tumefanikiwa kutengeneza sehemu ya watoto ya michezo ambayo inawapa watoto furaha. Karibu sana uwalete watoto wako wacheze na kufurahi.
Usharika wa Kanisa Kuu ndio Kanisa Kuu la Dayosisi ya Mwanga. Kanisa hili liko Mwanga mjini na linatoa huduma zote za kikanisa, na ndipo kiti cha Baba Askofu kilipo. Tunatoa huduma za ibada kila Jumapili na kati ya wiki kila asubuhi saa kumi na mbili.
Ibada za Jumapili ziko tatu, ya kwanza inaanza saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili na nusu, ya pili inaanza saa moja na nusu hadi saa tatu na ibada ya tatu inaanza saa nne hadi saa tano na nusu.
Ibada ya saa nne ni kwa ajili ya vijana zaidi ila pia hata watu wazima wanahudhuria. Tunaiita "Ibada ya Vijana".
Mazingira ya kuvutia katika Bustani yetu,kuna maeneo ambayo unaweza kuja kufanya shughuli mbalimbali kama :- kumbukizi ya siku ya kuzaliwa , Send Off, Engagement ,Harusi pamoja na mengine ya nayo fanana nashughuli hizo. Karibuni sana nyote mnakaribishwa.
Ukiwa katika Duka letu la vitabu utajipatia vitabu mbali mbali kwa bei nafuu kabisa, lengo nikusaidia jamii kupata kilicho bora lakini zaidi kuandaa au kuendeleza Taifa lilo bora na lenye baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mhe. Baba Askofu Chediel Elinanza Sendoro Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga akikabidhi zawadi ya Kondoo ilionunuliwa na washarika kwa Mgeni Rasmi.Mhe.. Deogratius J. Ndejembi Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI ambapo ameshiriki Ibada ya uzinduzi wa Harambee ya Maendeleo KKKT Dayosisi Ya Mwanga akimuakilisha Waziri wa Fedha wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.. Mwigulu Nchemba.
Copyright © 2021 - All Rights Reserved - Mwanga Diocese (ELCT.MWD)