Tel: +255752115528| Mail: info@elctmwd.org




   MWANGA BOOK SHOP         OUR PARTNERS   

KIWANDA CHA MAZIWA USHARIKA WASHIGHATINI

Hiki ni Kiwanda ambacho kipo katika hatua za mwisho kabisa katika muendelezo wa taratibu za ukamilshaji wa baadhi ya vifaaa ilikiweze kuanza kzi. Kiwanda hiki ni moja ya miradi ya maendeleo katika usharika wa Shifghatini lakini pamoja na KKKT Dayosisi ya Mwanga kwaujumla wake. ...



MWANGA LUTHERAN HOSTEL

karibu wote...amani na upendo...



MWANGA LUTHERAN HOSTEL

Hosteli yetu ya Mwanga kuwa sehemu moja wapo yakutoa huduma kwa jamii kwakuzingatia huduma zote muhimu ambazo mgeni atakaye fika anaweza kupata huduma pasipo usumbufu lakini pia mgeni au mteja atakapo kuwa katika hosteli yetu atafurahia pia huduma zinazo tolewa ndani ya hosteli hii pamoja na mazingira mazuri yanayo mzunguka. Unaweza kujiuliza au kuuliza kwanini au sababu gani ya kujenga hosteli hii hapa Mwanga. Utalii ni chanzo kizuri sana cha mapato hapa Tanzania pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro wilayani Mwanga ukizingatia kuwa sehemu ya hifadhi ya taifa ya wanyama ya Mkomazi ambayo inapatika Mwanga. Kuna hoteli na nyumba za wageni nyingi lakini wageni wanahitaji sehemu ambayo ni nzuri, yenye mazingira mazuri ya kuvutia ambayo ni tofauti na sehemu zingine, sehemu ambayo wataikumbuka na kuwaambia marafiki zao waitembelee kutokana na huduma bora zinazo patikana au kutolewa katika hosteli hii. Lakini niwazi kwamba Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wamekuwa na ushirika au ushirikiano wa karibu sana na ndugu zetu kutoka nchini Ujerumani katika masuala mbalimbali ya Kanisa. Uwepo wa hosteli hii ni pamoja na ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa ndugu zetu Wajerumani. Kwa maana hiyo hatuna budi kusema ndugu zetu wote Kutoka Ujerumani lakini pia Familia rafiki kutoka nchi zingine pamoja na wageni wa ndani tuna wakaribisha katika hosteli yetu kwa ajili ya kupata huduma bora kabisa lakini zaidi kufurahia Mandhari au mazingira yetu yanayo tuzunguka hapa nyumbani Mwanga pamoja na Vivutio vyake vilivyopo kama hifadhi ya Taifa ya Mbuga ya wanyama ya Mkomazi. Hosteli yetu ina vitanda, magodoro mazuri, shuka nzuri na safi, vyakula vizuri na vitamu tofauti na mahali pengine, huduma nzuri na ya kuvutia, bustani nzuri na mazigira mazuri tulivu ya kuvutia yanayowafanya wajisikie vizuri, hata kama mgeni anaharaka amekuja kunywa kahawa ajisikie kukaa zaidi na atamani kurudi tena. ...



MWANGA LUTHERAN KIDS PLAYGROUND

Mwanga Lutheran Kids Playground ni eneo maalum kwaajili ya michezo ya watoto, katika eneo hili la kuna michezo mbambali ya watoto ambayo ambayo itamfanya mtoto /watoto kujiweka sawa katika utimamu wa akili lakini kwa afya pia. Tuna wakaribisha wazazi walezi kwaaji ya kuleta watoto wenu katika maeneo yetu ya michezo siku za mapumziko ilikuja kufurahi na kucheza pamoja na familia zenu . Karibuni sana. ...



MFUKO WA KUDUMU WA MAENDELEO YA DAYOSISI LIPA NAMBA :  3 2 3 2 1 1   ELCT-MWANGA DIOCESE [ VODACOM ]