Tel: +255752115528| Mail: info@elctmwd.org
   MWANGA BOOK SHOP         OUR PARTNERS   


MWANGA DIOCESEDayosisi ya Mwanga imezaliwa kutoka Dayosisi ya Pare, ikiwa ni Dayosisi ya 25 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Dayosisi Hii ilizinduliwa rasmi na Mhe. Askofu Dr. Fredrick Shoo mnamo tarehe 6 November 2016; ikiwa imeanza na jumla ya idadi ya washarika 26,000 ambao walikuwa wakitunzwa na sharika 21 na mitaa 66 kabla sharika pamoja na mitaa mingine kuongezeka.

Mara baada ya Dayosisi ya Mwanga kuzaliwa au kuanzishwa Askofu mwanzilishi, Mchungaji Chedieli Elinaza Sendoro aliwekwa wakfu na kuanza majukumu yake ya kazi siku hiyi hiyo ya Tarehe 6 Novemba 2016.

Historia ya Kanisa la Kiinjili katika ukanda huu wa Pare au Vwasu ilianza mwishoni mwa karne ya19, baada ya wamisionari wa Kijerumani kutoka chama chama cha Misioni Cha Kilutheri cha Leipzig(LeipzigLutheran Missionary Society)walipofika nakuanzisha kituo kikuu cha kwanza cha Misioni Shighatini Ugweno.

Mmisionari wa kwanza au mtangulizi, Mchungaji Hans Fuchs ambae wapare walimuita (Bwana Fukudha )akitokea kituo cha misioni cha Mamba Uchagani, alifika Shighatini akasimika hema la kwanza katika ardhi ya Pare mnamo tarehe 11 mwezi julai mwaka 1900.

Pamoja na kufundisha Neno la Mungu , alianzisha shule na kufundisha watoto kusoma ,kuandika pamoja na Hesabu; alianzisha huduma ya utabibu katika zahanati , alitengeneza barabara ,alifundisha masuala ya kilimo cha kisasa pamoja na biashara , Usafi na Maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kutokana na juhudi zake Mmisionari Hans Fuchs na wenzake , na kwa jinsi wenyeji walivyo wapokea kwa ukarimu wamisionari hawa, Neno la Mungu pamoja na maendeleo vilichanua na kuenea Pare /Vwasu yote.

Waumini wa Kilutheri wa Mwanga ni sehemu kubwa ya utajiri wa historia ndefu ya ukuaji na mabadiliko ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, kutoka mwanzo mdogo kama Kituo cha Misioni Shighatini na kuwa sehemu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanganyika Kaskazini mnamo mwaka 1937, na Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika mwaka 1938, Dayosisi ya Kaskazini ya kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania KKKT mwaka 1963, na KKKT Dayosisi ya Pare iliyozaliwa mwaka 1975 kutoka KKKT Dayosisi ya Kaskazini na hatimaye KKKT Dayosisi ya Mwanga iliyozaliwa /kuanzishwa kutoka KKKT Dayosisi Ya Pare Mwaka 2016.


ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA MWANGA

RT. REV. CHEDIEL ELINAZA SENDORO

MSAIDIZI WA ASKOFU KKKT DAYOSISI YA MWANGA

MCH. TIMOTHY JONAS MSANGI


MAJIMBO YALIYOPO DAYOSISI YA MWANGA

JIMBO MKUU WAJIMBO         CONTACT        
JIMBO LA TAMBARARE MCHG. MBONEA MFWANGAVO 0758 419 471   VIST  
 
JIMBO LA MAGHARIBI MCHG. JOSEPH MCHOMVU 0657 487 610   VIST  
 
JIMBO LA MASHARIKI MCHG. BILLY-GRAHAM MSANGI 0752 443 201   VIST