-
MWANGA BOOK SHOP
OUR PARTNERS
USHARIKA WA KANISA KUU
Usharika wa Kanisa Kuu ndio Kanisa Kuu la Dayosisi ya Mwanga. Kanisa hili liko Mwanga mjini na linatoa huduma zote za kikanisa, na ndipo kiti cha Baba Askofu kilipo. Tunatoa huduma za ibada kila Jumapili na kati ya wiki kila asubuhi saa kumi na mbili.
Ibada za Jumapili ziko tatu, ya kwanza inaanza saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili na nusu, ya pili inaanza saa moja na nusu hadi saa tatu na ibada ya tatu inaanza saa nne hadi saa tano na nusu.
Ibada ya saa nne ni kwa ajili ya vijana zaidi ila pia hata watu wazima wanahudhuria. Tunaiita "Ibada ya Vijana".