
MWANGA DIOCESE

Kwenye picha ni wachungaji sita walio barikiwa siki ya Bwana ya Watakatifu wote kwenye Usharika wa Kanisa Kuu Dayosisi ya Mwanga. Dayosisi tatu ziliungana kwa pamoja katika kuwabari wachungaji hawa kutoka Dayosisi ya Mwanga, Dayosisi ya Same na Dayosisi ya Karagwe yafuataayo ni majina ya wachunga walio barikiwa siku uyo Mchg David John -Dayosisi ya Mwanga Mchg Simon Yohana Oyaya -Dayosisi ya Mwanga Mchng Petro Godbles Kowero -Dayosisi ya Mwanga Mchng Lida Stephano Elia -Dayosisi ya Mwanga Mchng Naomi kutoona -Dayosisi ya karagwe Mchng Rehema Mkumbwa- Dayosisi ya Pare ....

Askofu wa kanisa la Katoliki Jimbo la Same (Rt- Rogath Kimaryo )akiambatana na watawa wa Kanisa Katoliki jimbo la Same katika ibada ya kubariki Wachungaji sita wa Dayosisi ya Mwanga, Dayosisi ya Same na Dayosisi ya Karagwe pamoja na Ibada ya shukrani ya Miaka sita ya Dayosisi ya Mwanga toka kuanza Kwake. Askofu Rogath Kimaryo alipata nafasi ya kuzungumza nawaumini wa KKKT na wote walio udhiria Ibada hiyo ambapo alisisitizia dhana ya umoja katika Kuifanya kazi ya Bwana .Pia alizungumza watu wawe na bidii ya kujituma zaidi katika Kumjuwa Mungu na alitowa ujumbe wa neno la Mungu kutoka kitabu cha Wafilipi 4:13 (Tazama nayaweza yote katika yeye anitiaye Nguvu)....

Baba Askofu Dkt Alex G. Malasusa (Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani )kulia na kushoto ni Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Askofo CHEDIEL Elinanza Sendoro kwa pamoja walishirikiana kuongoza ibada ya uzinduzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Dayosisi ya Mwanga. Ambayo yamezinduliwa siku ya Bwana ya Watakatifu wote. Sambamba na uzinduzi huo Kulikuwa na ibada maalumu ya kubariki Wachungaji sita wa Dayosisi ya Mwanga, Same na Karagwe pamoja na ibada ya shukrani kwa Dayosisi ya Mwanga kutimiza miaka sita toka kuanzishwa kwake ....